UHAMASISHAJI WA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

08/03/2024
Na Kadzo Purity
Huku ulimwengu ukisherehekea siku ya mwanamke dunia almaarufu “ international women's day”. Wengi wa wanawake hao pamoja na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za mwanamke yamejitokeza kutetea haki za wasichana wadogo ambao haki zako zimekua zikikiukwa kwa muda sasa hususan wameonekana wakipinga vikali swala la mimba za mapema ambalo limekua donda sugu nchini.

Kulingana na taarifa za hivi majuzi, shirika la kutetea haki za mwanadamu(KHRC), ilibaini kwamba kumekua na ongezeko la mimba za utotoni katika baadhi ya kaunti.
Kaunti ya Nairobi ndio kaunti inayoongoza na idadi kubwa ya mimba za utotoni.
Nairobi - 452
Kakamega-328
Bungoma- 294
Nakuru- 283
Kilifi- 224
Meru- 206
Kisii- 192
Machakos- 178
Narok- 176

Hatahivyo shirika hilo la kutetea haki za binadamu limedai kwamba sababu za ongezeko la mimba hizo za utotoni limechangiwa na umaskini , dhuluma za kijinsia, elimu duni, tamaduni hasi zilizopitwa na wakati pamoja na likizo ndefu.

Ni wazi kwamba ili kutatua jambo hili basi serikali za kaunti zinafaa kujukumika kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa mwanamke na madhara ya watoto kupata ujauzito katika umri mdogo.
© 2024 Unity Media 254. All rights reserved.
Powered by Webnode Cookies
Create your website for free! This website was made with Webnode. Create your own for free today! Get started